Monday, May 07, 2012

"Toa Kitabu Kisomwe"-Ombi toka UDI

Asasi ya Maendeleo Ubungo (Ubungo Development Initiative-UDI) imezindua Programu ya Taarifa yenye ujumbe “Toa Kitabu Kisomwe” inayohusisha kukusanya vitabu vya kiada na vya ziada kutoka wa watu mbalimbali na taasisi mbalimbali na kuvisambaza katika taasisi za elimu kwa ajili ya wanafunzi kusoma na maeneo maalumu kwa ajili ya wananchi kujisomea. Tunaomba taasisi au mwananchi yoyote mwenye kitabu chochote popote ambaye yuko tayari kukitoa ili kisomwe iwe ni cha kiada au cha ziada awasiliane UDI ili iweze kufikisha kitabu hicho kwa walengwa. “Toa kitabu kisomwe” kupitia ofisi ya UDI iliyopo Kimara Kona au wasiliana na Ubungo Development Initiative (UDI) kupitia Afisa Taarifa (0768503331 au 0715745874) au barua pepe ubungo2005@yahoo.com kutoa kitabu husika. Ukipenda unaweza kuweka saini kwenye kitabu hicho kama kumbukumbu kuwa taasisi yenu au wewe ndiye uliye “Toa kitabu Kisomwe” au unaweza pia kutueleza kitabu hicho unapendekezwa kipelekwe wapi ndani ya Manispaa ya Kinondoni ili kiweze kusomwa kwa ufanisi. Sisi mpango wetu ni kusambaza vitabu hivyo kwenye maktaba za shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kwa upande wa elimu ya kiada na kusambaza kwenye maktaba za jumuia, ofisi za serikali za mtaa, taasisi za kijamii na vijiwe vya kudumu kwa upande wa elimu ya ziada. Tunaamini kwamba kwenye kaya mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni vipo vitabu makabatini au masandukuni ambavyo ama ni vya kiada vilivyoachwa baada ya walengwa wa awali kupanda ngazi moja ya elimu kutoka ile ambayo walikuwa wakisoma au ni vya ziada ambavyo tayari wahusika walishavitumia na vinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa walengwa wengine wenye kuvihitaji hivyo; “Toa Kitabu Kisomwe”. Aidha, tunaamini pia kwamba Jiji la Dar es salaam lina makao makuu ya taasisi mbalimbali ambazo hutoa vitabu mbalimbali kwa ajili ya kusambaza nchini lakini wakati mwingine hushindwa kuwafikia walengwa katika ngazi ya chini jijini hivyo UDI kwa kuwa taasisi ya ngazi ya chini inaweza kuwa kiungo kizuri cha kuwezesha vitabu husika kuwafikia walengwa; “Toa Kitabu Kisomwe”.

Wednesday, March 24, 2010

UDI provides platform for community service

Ubungo Development Initiative (UDI) is a civil society organization established and registered in Tanzania in 2006. The founders of the organization realized during 2005 that development of the constituency can be expedited with good leadership and responsible citizenry that necessitate civil society advocacy and community service.

UDI apart from implementing projects that are supported by development partners it also provide platform for individuals to do community work through the organization. So feel free to contact us via ubungo2005@yahoo.com if you wish to save or serve society. Thank you for your support.

Details on UDI’s objectives are available at: http://ubungo.blogspot.com/2006/10/udi-intro.html

Wednesday, May 28, 2008

Muktasari na Maazimio ya Semina ya Wakazi Kibamba

MUHTASARI NA MAAZIMIO YA SEMINA YA WAKAZI WA KATA YA KIBAMBA ENEO LA LUGURUNI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI KATI YAO NA SERIKALI KUHUSIANA NA MRADI WA MJI WA MFANO WA LUGURUNI.

TAREHE YA SEMINA : 24/05/2008
ENEO LA SEMINA: UWANJA WA MPIRA KIBAMBA ZAHANATI

UTANGULIZI:

Tatizo la msongamano wa magari na watu katikati ya jiji la Dar es Salaam halikuanza leo. Katikati ya miaka ya 90 hatua kadhaa zilianza kuchukuliwa na serikali ili kupunguza na hatimaye kuondoa tatizo hilo. Moja ya mikakati kabambe ilibuniwa na Tume ya Jiji iliyoundwa mahsusi kushughulikia matatizo ya utoaji huduma kwa wakazi wa jiji kutoka serikalini kwenda kwa wananchi. Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mheshimiwa Charles Keenja, ambaye sasa ni mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Ubungo, lililo na kata 11, Kibamba ikiwemo, ilikuja na mbinu za kujenga barabara za pembezoni zikiunganisha votongoji kadhaa bila kupitia katikati ya jiji. Mpango huu ulionyesha mafanikio kwani msongamano ulidhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, kufuatia sera ya biashara huria kukubaliwa nchini, idadi ya magari yaliyoingizwa nchini iliongezeka kwa kasi kubwa na hivyo kushinda ujenzi wa barabara hizo, na kulifanya tatizo kukua. Idadi ya watu nayo iliongezeka kwa kasi kubwa kufuatia hali duni ya huduma huko mikoani, na vijijini hivyo kuwafanya watu wengi kukimbilia jijini ili kujitafutia riziki na kuboresha maisha yao.

Serikali ilianza kujizatiti ili kukabiliana na msongamo wa watu na magari , kwa kuchukua hatua mbalimbali kama ya hivi karibuni ambapo aliyekuwa waziri mkuu, Mheshimiwa Edward Lowassa alibuni mpango wake wa kuruhusu magari kutofuata sheria za barabarani ili kupunguza msongamano. Mpango wake huu unajulikana kama Njia Tatu. Madhara kadhaa yakiwemo vifo kwa wananchi yametokea, na yanaendelea kutokea kufuatia utekelezaji huo wa amri ya Mheshimiwa Lowassa. Hadi sasa, serikali haijatoa msimamo wake rasmi kuhusu faida au hasara za mpango wa njia tatu, kama unakubalika kisheria na kama utaendelea kwa muda gani.

Serikali pia ilibuni mpango wa kujenga miji midogo yenye hadhi pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam ili kupunguza idadi ya watu wanaokwenda kufuata huduma katikati ya jiji. Moja ya mji huo wa mfano uliobuniwa na serikali ni Luguruni, uliopo kiasi cha kilometa 25 kutoka Dar es Salaam kuelekea Kibaha, mkoani Pwani. Eneo la Luguruni lipo ndani ya Kata ya Kibamba, Manispaa ya Kinondoni.Tathmini ya kwanza ilifanyika Juni mwaka jana.

Hata hivyo tangu serikali kuanza kuzilipa fidia familia 259 zinazohusika katika eneo hilo la mradi lenye ukubwa wa hekta 54, kumekuwepo na malalamiko mengi yaliyowahusisha watendaji wa serikali ya mtaa na kata ya Kibamba , manispaa ya Kinondoni na wizara ya Ardhi nyumba na makazi waliokuwa wasimamizi wa mradi huo. Tuhuma kadhaa za rushwa, uonevu, upendeleo na kutokuwajibika kwa viongozi hao ndiyo chanjo cha mgogoro huu.

MAHUDHURIO :

Katika semina hiyo iliyoitishwa na asasi ya kiraia ya Maendelo Ubungo( Ubungo Development Initiative,UDI) ikishirikiana na kikundi cha wananchi wa Kibamba Luguruni cha maendeleo na Uchumi(WAKILUKI) ilihudhuriwa na wananchi wapatao 125 kutoka maeneo mbalimbali ya kata ya Kibamba.Taarifa zisiso rasmi zilieleza kuwa baadhi wa wananchi walitishwa kuhudhuria kwamba polisi walikuwa wamejiandaa kuwakamata viongozi wa semina hiyo pamoja na wananchi watakaohudhuria kwani haikuwa na baraka za serikali, hivyo kuwa batili.

Kilichowasikitisha wananchi waliohudhuria semina hii ni kuona kuwa hakuna kiongozi wa wananchi hata mmoja aliyehudhuria wala kutoa udhuru wa kutokuhudhuria. Viongozi walioalikwa na ambao hakuna hata mmoja aliyehudhuria ni
1. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kibamba
2. Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kibamba
3. Afisa Mtendaji wa Kata ya Kibamba
4. Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kibamba
5. Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Ubungo.
Viongozi hawa licha ya kupelekewa mialiko rasmi ya kuhudhuria semina hii muhimu ya wananchi ili wasaidie kujibu baadhi ya hoja za msingi, kuwaelekeza wananchi kwenye ufumbuzi wa tatizo hili na kujifunza kutoka kwa watoa mada waliamua kususia bila kutoa sababu zozote.

Pamoja na hali hiyo, wananchi waliohudhuria semina hiyo walikaa kwa utulivu na kuchangia katika kila mada kiasi cha kuifanya semina kuwa ya kufurahisha. Semina ilianza saa 4 asubuhi hadi saa 9 mchana.


MADA ZA SEMINA:
Mada muhimu zilizojadiliwa kwa pamoja kati ya waandaaji wa semina na wananchi ni pamoja na :
1. Ufafanuzi wa sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 179.
2. Tangazo la serikali kuhusiana na masuala ya ardhi namba 78 la mwaka 2001
3. Mtiririko wa malipo halali ya fedha za serikali
4. Sera ya taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi vifungu vya 4.9.1 hadi 4.9.3

Mada hizi zilijadiliwa kwa kina na kuchambuliwa kwa madhumuni ya kueleweka vizuri na wananchi wote. Wananchi wengi walikubali kuwa kuna upungufu mkubwa wa taarifa, sera, sheria na baadhi ya taratibu za serikali kutokueleweka kwao, na hicho ndicho kikwazo kikubwa na mbinu zinazofanywa na baadhi ya viongozi wabadhirifu kuwahadaa wananchi kwa kutokuzijuwa.

Baadhi ya vifungu muhimu vya sheria hii vilivyojadiliwa kwa kina ni pamoja na kile kinachoeleza bayana kuwa endapo serikali itaamua kuchukuwa eneo la mwananchi kwa ajili ya shughuli za kijamii, kwa manufaa ya umma, basi serikali italazimika kumshirikisha mmilikajiwa eneo hilo katika mchakato wa kufikia makubaliano ya fidia tangu mwanzo hadi mwisho, na kwamba malipo halali yaliyokubaliwa na wadau wote wawili yatafanyika mapema na kwa haki bila kumsababishia mwananchi huyo adha yoyote. Wananchi walisema kuwa kilichofanyika na serikali mkatika mradi huu ni tofauti na sheria zake yenyewe, kwamba hawakushirikishwa katika hatua yoyote ya tathmini hadi malipo, na ndiyo maana kuna malalamiko mengi. Waliongeza kuwa serikali iliwahadaa wananchi kwa kuwaambia kuwa watalipwa vizuri, bila kuwatajia njia watakazotumia kufikia kiasi cha malipo husika.

Katika uchambuzi wake mmoja wa watoa mada, Ndugu Chrisant Kibogoyo aliwaeleza wanasemina kuwa sheria ya fidia inatamka wazi kuwa :
• Fidia ni kwa bei ya soko la sasa
• Baadhi ya posho zinazoambatana na fidia ni
i) posho ya usumbufu
ii) posho ya makazi, ambayo ni bei ya kupanga nyumba kama inayolipiwa fidia katika eneo hilo
iii) posho ya usafiri wa mizigo kiasi cha tani 12 kwa kilometa 20
iv) posho ya upotevu wa faida iliyokuwa ikipatikana kutokana na mali inayolipiwa fidia.
• Utaratibu wa malipo ya fidia ya serikali unatumia fomu maalumu mbili, moja nyeupe na nyingine ya bluu. Hapa alifafanua kuwa kama kuna mwananchi aliyefanyiwa tathmini na kulipwa pesa bila kujaza na kusaini fomu hizo, basi malipo yale hayakutoka serikalini kwa kuwa serikali ni makini sana katika kufuata taratibu. Alidokeza kuwa kinachopangwa kufanyika sasa ni kuwahadaa wananchi wote waliolipwa kinyume na taratibu kukubali kuzijaza kinyemela ili kuhalalisha malipo hayo. Aliwatahadharisha wananchi kuwa macho na ujanja huo kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya wapoteze haki zao. Kimsingi alisema kuwa inavyoonekana mradi huu wa mji wa mfano wa Luguruni labda siyo wa serikali bali wa wawekezaji fulani waliotumia mgongo wa serikali kuwaibia wananchi haki zao.Aliendelea kusema kuwa kwa jinsi anavyoifahamu serikali isingeweza kuwafanyia tathmini wananchi kwenye daftari( counter book) badala ya fomu maalumu ambazo serikali yenyewe ndiyo iliyozitengeneza ili zitumike nchi nzima kufanya tathmini.

Mtoa mada mwingine ambaye amesomea masuala ya uhasibu na ambaye amefanya kazi serikalini aliwaeleza wanasemina taratibu za malipo ya fedha za serikali kama ifuatavyo:

i)Chanzo cha madai kiwepo, kikiwa kimejazwa kwa usahihi( Proforma Invoice)
ii) Mtu wa kuanza mchakato wa malipo ya fedha za serikali atambulikane kwa jina na cheo chake
iii) Ukaguzi wa ofisa wa ngazi ya juu wa fomu ya chanzo cha madai ufanyike ili kujiridhisha kuwa fomu hiyo ni halali na imezajwa ipasavyo
v) Fomu hiyo iidhinishwe na ofisa mwingine anayetambulika na serikali kuwa yote yaliyomo ni sahihi kwa kadri ya uelewa wake
vi) Muandaaji wa malipo kwa hundi atie saini yake, muidhinishaji naye atie saini yake, na mlipaji pia atie saini yake.
vii) Malipo hayo yaambatanishwe na fomu inayoeleza sababu za malipo, fungu zilipotoka , jina na anuani ya mlipwaji na akaunti ya benki malipo yatakapotolewa.
viii) Kitabu maalumu cha kukabidhi hundi kitumike ( cheque register book) kikionesha jina la mlipwaji, kiasi cha malipo, namba ya cheki inayolipwa, na mlipwaji atie saini yake kuwa amepokea malipo.

Mtoa mada alisisitiza kuwa kama taratibu kama hizi hazikufuatwa wakati wa mchakato mzima wa kuandaa hadi kulipa fidia, basi kutakuwa na walakini katika malipo hayo. Aliongeza kuwa kimsingi, ni lazima kuwe na mkataba kati ya serikali na mlipwaji uliotiwa saini na wahusika wote wawili na kuthibitishwa na mwanasheria anayetabulika au hakimu anayefanya kazi serikalini, na kuwekwa muhuri . Hii ni hati ya kumbukumbu kwa kila mmoja wa walioingia mkataba ili pakitokea kutokuelewana baina yao warejee kwenye vifungu vya makubaliano yao.





MICHANGO KUTOKA KWA WANASEMINA:
• Pamoja na waziri Chiligati kusema kuwa tathmini itafanyika upya bado kuna tetesi kuwa viongozi wa mtaa wanawatumia wajumbe wa nyumba kumi kuwahadaa au kuwatisha wahusika kutokuhudhuria semina wala mikutano itakayoitishwa na watu wengine kuhusu mgogoro huu.
• Kwa wale waliolipwa tayari marekebisho yafanyike kulingana na sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 pamoja na fidia zote kulingana na bei ya soko.
• Mafunzo ya sheria , haki za binadamu na somo la uraia yafanike kila mtaa ili kuwaamsha wananchi wasiendelee kuminywa na viongozi wabadhirifu . Asasi za kiraia kama UDI na KIWALUKI ziwezeshwe kuendeleza mafunzo haya.
• Ubaguzi wa vyama vya siasa na dini vikemewe ili kuwaunganisha wananchi kwa ajili ya maendeleo yao. Baadhi ya viongozi wa CCM walio madarakani wanatumia suala la siasa kuwatenga wananchi ili wasielewe kinachoendelea.
• Viongozi waache kulindana kwa visingizo kuwa hakuna ushahidi wa kutosha. Malalamiko ya wananchi yakiwa mengi kwa kiongozi mmoja yatumike kama ushahidi wa kutoa madarakani
• Tathmini ya ardhi ya Kibamba izingatie bei ya soko la sasa ambapo kiwanja chenye ukubwa wa mita 20 kwa 20 kinauzwa kwa shilingi milioni 5.
• Wafanyakazi wote wa ardhi wakiwemo wa serikali ya mtaa na kata ya Kimbamba waliotuhumiwa na majina yao kukabidhiwa kwa Magufuli wasionekane kuhusiika na tathmini mpya kama itafanyika.
• Viongozi wa mtaa na kata waliokwepa kuhudhuria semina hii washinikizwe kuwaeleza wananchi sababu za kukataa kuhudhuria huku wakiwa ndiyo viongozi wanaotegemewa na wananchi.
• Viongozi wa kata na wilaya wanaoeneza uvumi kuwa Kibamba kuna kikundi cha kigaidi na wanasiasa uchwara watoe uthibitisho kwenye mkutano wa wananchi. Ilielezwa kuwa mnamo tarehe 8/ 5/2008 katika mtaa wa Kibwegere, mkuu wa wilaya ya Kinondoni Kanali Massawe alikwenda kuwahutubia wananchi wapatao 50 na kuwaambia kuwa:
i) Wananchi wa Luguruni na kwembe wamezuia mradi wa maendeleo wa Luguruni uliobuniwa na kufadhuiliwa na serikali
ii) Kuna kikundi cha wanasiasa uchwara na cha kigaidi cha KIWALUKI kinachohusika na kuwadanganya wananchi
iii) Kwamba kikundi hicho kilimsomea Mkuu wa Wilaya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi risala ya kutisha. Wananchi walisikitishwa na taarifa hizo potofu na kumtaka mkuu huyo awaombe radhi wananchi wa Kwembe na Luguruni kwa upotoshaji huo. Wao walisema kuwa hawajazuia mradi licha ya kutaka walipwe haki zao kulingana na sheria. Walisema kauli kama hizo za uongo zinazotolewa na viongozi wakuu wa Wilaya zinaonesha kuwa baadhi ya viongozi hawafanyi kazi kwa maslahi ya wananchi ila kwa kuwakumbatia viongozi wabovu na kuwadharau wananchi.Walegusia toleo la gazeti la Mtanzania la tarehe 30/4 2008 ambapo mkuu huyo wa wilaya alisemekana kumdanganya waziri kiasi cha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kumbana ili aseme ukweli. Walisema inaelekea mkuu huyo wa wilaya ana makusudi mengine na siyo kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.
Baada ya michango mingi kupokelewa kutoka kwa wanasemina na kujadiliwa, wote walikubalina na dhana ya kutoa maazimio ambayo waliomba yafikishwe kwenye vyombo vya habari na Bungeni kupitia kambi ya upinzani kwa kuwa mbunge wao wa CCM Mheshimiwa Charles Keenja amedhihirisha kuwa hawathamini wananchi wake, wala hataki kujihusisha na mgogoro huu kama vile hauhusu. Wameomba wabunge wa kambi ya upinzani wapeleke kilio chao bungeni ili wabunge wote kwa pamoja wapendekeze njia bora ya kumaliza mgogoro huu.


MAAZIMIO YA WANASEMINA

Sisi Wananchi wa kata ya Kibamba, hususan wakazi wa eneo la Luguruni, baada ya kuhudhuria semina hii na kujadiliana kwa kina baadhi ya matatizo yanayosababisha mgogoro kati yetu na serikali kuhusu malipo ya fidia tunaazimia kama ifuatavyo:-

i) Semina za namna hii zinazotoa mwanga wa elimu juu ya haki zetu na kutupatia fursa ya kutoa dukuduku zetu kwa uwazi na bila hofu ziendelee kutolewa na asasi za kiraia pamoja na serikali yetu .
ii) Elimu kwa umma kuhusu sera, kanuni na sheria mbalimbali za nchi yetu zisiishie kuwekwa kwenye makabati ya idara za serikali, badala yake zitawanywe kwa wananchi, asasi za kiraia na hata katika mtandao wa Intaneti ili wananchi wengi zaidi wanufaike nazo.
iii) Wakati wa semina kama hizi, wabunge wote wa Wilaya ya Kinondoni, bila kujali wanatokana na chama kipi cha siasa, wahudhurie ili panapotokea hoja za kisera na kisheria wazinukuu na kuzifanyia kazi huko bungeni kwa manufaa ya wananchi
iv) Katika mradi huu wa Luguruni kama wapo wawekezaji nje ya serikali wajitokeze ili wakutane na wananchi wanaohusika na kujadiliana jinsi ya kuendeleza mradi huu kwa pamoja, badala ya kujificha mgongoni mwa watendaji wachache wa serikali. Kama ni serikali yenyewe, basi itumie haki kuwalipa wananchi ili mradi uanze na kukamilika kwa wakati.
v) Hesabu kamili za wanaopaswa kulipwa fidia , waliokwisha kulipwa, na ambao hawajalipwa iwekwe wazi katika mbao za matangazo ili wananchi wazipitie , kuzikagua na kuwatambua waliolipwa isivyo halali.
vi) Pamoja na kuwalipa wahusika, serikali ifikiria upya uamuzi wake wa kumtaka kila aliyelipwa kubomoa nyumba yake kwani kuna baadhi ya majengo ambayo yakibakia yanaweza kutumika kama maghala ya kuhifadhi chakula, mizigo na kadhalika.matumizi bora ya fedha za umma yazingatiwe katika zoezi hili.
vii) Sheria zinazowalinda viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wasiowajibika kuendelea kubakia madarakani hadi uchaguzi mwingine zifikiriwe upya, au kama kuna njia ya kuwaondoa viongozi hao zijulikane ili wananchi wazitumie kuwaadabisha.
viii) Demokrasia inaonekana kutokuwepo Kibamba. Tunaiomba serikali irudishe demokrasia Kata ya Kibamba ili wananchi wahudumiwe na viongozi badala ya viongozi kuwakandamiza wananchi.
ix) Miradi ya serikali isimamiwe na viongozi wa serikali badala ya wajumbe wa nyumba kumi ambao ni viongozi wa kisiasa. Wananchi watambulishwe kwa watendaji kabla ya kuanza kazi ili wawatathmini juu ya utendaji wao.
x) Viongozi waliokataa kuhudhuria semina watoe sababu mbela ya mkutano wa wananchi wote utakaoitisha karibuni.

Wednesday, April 16, 2008

Mjadala wa Maendeleo Ubungo-12 April 2008

Mjadala wa Maendeleo Ubungo ulikwenda vizuri tarehe 12 Aprili 2008. Watoa mada siku hiyo walikuwa ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni(huduma zitolewazo na manispaa); Mstadi toka kampuni ya TESTA(Huduma zitolewazo na asasi za kiraia) na Mmoja wa waasisi wa UDI. Mkurugenzi wa UDI naye alihutubia siku hiyo. Tutawaletea mada za wazungumzaji wote pamoja na ripoti ya mjadala huo ikiwa tayari. Kwa leo, tuwawekee mada moja wapo:

Mada iliyowasilishwa kwenye Mjadala wa Maendeleo-Jimbo la Ubungo uliofanyika katika Ukumbi Wa Land Mark Hotel, Ubungo-Dar es salaam. Mwandishi wa mada hii ni mwanaharakati, mkazi wa jimbo la Ubungo na mmoja ya waasisi wa Asasi ya Maendeleo Ubungo (UDI) anayepatikana kupitia 0754694553 na mnyika@yahoo.com


USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA KULETA MAENDELEO

“MISINGI 25”

Na John J. Mnyika

Mada hii imeandaliwa kwa ufupi kuchochea fikra na mjadala kuhusu “Ushiriki wa Wananchi Katika Kuleta Maendeleo”; na haki/wajibu katika muktadha huo hususani kwa viongozi na wananchi wa Jimbo la Ubungo.

Yapo masuala na mahitaji mengi ambayo kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuyafanya katika kuleta maendeleo katika eneo lake.
• Eneo inaweza kuwa ni asasi/taasisi, kijiji/mtaa, jimbo/wilaya nk.
• Ieleweke kwamba maendeleo yanayozungumzwa hapa si maendeleo ya mtu binafsi bali ni maendeleo ya jumuia/jamii.
• Kiongozi na mwananchi wa jimbo la Ubungo anayelengwa hapa inaweza kuwa kiongozi wa asasi/kikundi, mwanaharakati wa kawaida, kiongozi aliyechaguliwa na wananchi(mfano mwenyekiti wa kijiji, diwani) nk.


Masuala na mahitaji hayo yako katika sehemu kadhaa mathalani haki, wajibu, zana, mikakati, maangalizo, dondoo, stadi, mazingatio, shughuli na kadhalika. Mada hii imeyaweka pamoja masuala na mahitaji hayo kwa pamoja katika mtiririko rahisi na kuyaita jina la pamoja “Misingi 25”. Hivyo misingi iliyoainishwa hapa ni sehemu ya mambo muhimu ambayo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuyafanya yaweze kumsadia katika kuleta maendeleo katika eneo lake.

Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuzingatia misingi ifuatayo ili kuleta maendeleo:

I. UPATAJI WA RASLIMALI: Upataji wa raslimali na suala la msingi ambalo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kulifahamu na kulitilia maanani. Hii ni kwasababu maendeleo huletwa na kuwekeza raslimali. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa afahamu aina, vyanzo na namna ya kupata raslimali. Raslimali ni pamoja na watu, fedha, vitu na hata mawazo. Vyanzo vya raslimali vyaweza kuwa wananchi, serikali, wadau wa kimaendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali nk. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ni vyema akawa na stadi au akatumia wenye stadi za uandishi wa miradi na ukusanyaji wa raslimali. Baadhi ya vyanzo muhimu vya kiserikali ni pamoja na: Pesa za Maendeleo (capital development fund) ambazo zinatolewa kwa idadi ya watu kwa wastani wa dola moja na nusu kwa kila kichwa katika kata; Pesa za PADEP-Participatory Agricultural Development Programme(hizi zinatolewa kwa ajili ya miradi ya kijamii na miradi ya vikundi); Pesa za VVU/UKIMWI kupitia TACAIDS; pesa za mradi wa elimu ya msingi-MMEM; pesa za mpango wa elimu ya sekondari-MMES, pesa za TASAF-miradi ya vijiji/mitaa na mikopo kwa vikundi na vyanzo vingine vingi. Hivi vinashindwa kutumika baadhi ya maeneo kutokana na kutokufahamika ama kutokufuatiliwa ipasavyo. Baadhi ya vyanzo vya washirika wengine wa kimaendeleo ni PACT, SATF, Foundation for Civil Society, GTZ, USAID, FHI, DFID, CARE nk. Kuna haja ya kufuatilia kujua taratibu za kupata ruzuku au kujenga ushirika na taasisi hizi.


II. USHAWISHI NA UTETEZI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na stadi za ushawishi na utetezi. Hizi ni zana muhimu sana kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kutekeleza wajibu wa kuleta maendeleo. Uzoefu unaonyesha kuwa kuna viongozi ama wananchi wa Ubungo ambao wameweza kuleta maendeleo katika maeneo yao kutokana na kutumia vizuri stadi hizi. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo unapaswa kuelewa kuwa ‘ukitaka kuwamba ngoma lazima uvutie upande wako’. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutumia kila fursa ya vikao na nafasi nyinginezo kushawishi miradi ya kimaendeleo kuelekezwa katika kufanyika katika eneo lake. Utetezi unahusisha pia kuweza kujenga hoja katika medani mbalimbali kwa niaba ya wananchi wenye matatizo mbalimbali. Stadi za ushawishi na utetezi zinawezesha kujua wajibu huu unatekelezwa namna gani.

III. UHAMASISHAJI NA KAMPENI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na ufahamu wa jinsi ya kufanya uhamasishaji na kampeni. Huu ni msingi muhimu katika kuunganisha nguvu za viongozi na wananchi kwa ujumla. Pia hii ni zana muhimu katika kutatua masuala yanayokabili halaiki ya wananchi yanayohusika na kubadili fikra na mitazamo. Mathalani Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo lazima awe mstari wa mbele katika kupiga vita UKIMWI. Pia awe mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza. Kufanya mikutano ya jumuia ni wajibu wa msingi wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kama sehemu ya kufanikisha malengo haya.

IV. UFAHAMU WA SHERIA ZA MSINGI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na ufahamu wa sheria za msingi. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo wananchi mara kadhaa wanamtegemea Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwapa mwelekeo katika maeneo hayo. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu sheria za msingi. Si lazima Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwa na ufahamu wa kina wa kisheria maana anaweza kutumia misaada mbalimbali ya kisheria katika masuala tata lakini unapaswa kufahamu masuala la msingi kwa ajili ya kutoa mwelekeo.

V. UFAHAMU WA SERA ZA MSINGI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu masuala ya msingi ya kisera. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu sera za kiserikali yanayogusa moja kwa moja makundi maalumu ama wananchi kwa ujumla katika eneo husika kwa kuwa ni msingi wa muhimu katika kuundaa miradi ya kimaendeleo na kujenga hoja za kupata raslimali katika maeneo hayo.

VI. UPANGAJI WA MIPANGO: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na stadi za msingi za kupanga mipango au kuwatumia vizuri wataalam. Baadhi ya stadi za msingi ni pamoja na maandalizi ya mapendekezo ya miradi, kuandaa mipango kazi na kutayarisha mipango kazi. Katika mazingira ya sasa, raslimali ziko nyingi na zinapatikana kwa ushindani. Uwezo wa kupanga mipango inayotimiza vigezo ni msingi muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweza kutelekeleza wajibu wa kuleta maendeleo. Pia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuielewa mipango iliyopo ikiwemo ya serikali ambayo inaigusa eneo lake kwa namna moja au nyingine.

VII. UPANGAJI WA BAJETI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuelewa michakato ya upangaji wa bajeti hususani bajeti. Hii ni kwa sababu bajeti ni zana inayoongoza mgawanyo na matumizi ya raslimali. Hivyo maendeleo ya eneo lake inategemea vilevile kiasi ambacho eneo husika linapangiwa katika bajeti za ujumla. Uwezo wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kushawishi bajeti kuelekezwa katika eneo lake inategemea ujuzi na ushiriki katika katua za muhimu za kupanga bajeti.

VIII. UUNDAJI WA ASASI NA VIKUNDI VYA MAENDELEO: Katika muelekeo wa sasa wa kimaendeleo vikundi vinachukuliwa na serikali na wadau mbalimbali kama njia ya msingi ya kuleta maendeleo hususani katika ngazi za chini. Hivyo katika kuzitumia fursa hizi ni muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwa na uwezo wa kuhamasisha vikundi vidogo vidogo kuundwa katika eneo lake hususani na wanawake na vijana. Vikundi vinaweza kuundwa kulingana na mahitaji lakini ni muhimu kukawa na vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na vikundi vya uzalishaji mali. Ni muhimu pia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwa na asasi ya kijamii(CBO) ya katika eneo lake ambayo atashiriki na kuitumia kama mwanya wa kuvuta raslimali ambazo ni mahususi kwa ajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali.

IX. KUTUMIA UZOEFU WA MAENEO MENGINE: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ni muhimu kuamua kwa dhati kutumia uzoefu wa maeneo mengine. Kuna msemo kwamba hakuna haja ya kugundua gurudumu kama gurudumu lipo tayari. Msemo huu unamtaka Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuchota uzoefu katika maeneo mengine. Yapo maeneo ambayo viongozi ama wananchi wa Ubungo wake wametekeleza wajibu wa kuleta maendeleo kwa namna ya kuigwa. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kubadilishana uzoefu na viongozi wa maeneo hayo ama kwa kutembelea au kwa mawasiliano au kwa kusoma ripoti mbalimbali za msingi.


X. KUTUMIA WANACHAMA: Pamoja na kutumia chama/kikundi/asasi kama taasisi. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo lazima aweke kipaumbele kuwatumia wanachama wa chama/kikundi/asasi. Hii ni kwasababu wanachama wana shauku ya ziada kushiriki katika kuhakikisha Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anafanikiwa ili chama/kikundi/asasi kiweze kujijengea heshima na kukubalika. Hivyo kushiriki katika shughuli za chama/kikundi/asasi ni hatua ya msingi kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweza kuwa karibu na wanachama na hatimaye wanachama kwa upande wao kuweza kujitolea katika kuwaunga mkono.

XI. KUTUMIA WATAALAMU: Si misingi yote iliyotajwa humu ambayo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo atakuwa na utaalamu. Hivyo ni muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuamua kwa dhati kuwatumia wataalam mathalani katika kuandaa mipango, kuandika miradi nk. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo asione aibu kuhusisha wataalamu.Kushirikisha wataalamu kamwe si ishara ya udhaifu wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo. Ni suala la mgawanyo wa majukumu kati ya yale ya kitaalamu na majukumu ya kawaida ya kiuongozi.


XII. KUTUMIA MAWASILIANO: Uwezo wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kutumia mawasiliano ni msingi muhimu katika kufanikishwa wajibu wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo katika kuleta maendeleo. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu njia mbalimbali za mawasiliano na jinsi ya kuzitumia kwa ufanisi. Njia rahisi tu kama kuandika barua kwa mamlaka zinazohusika na wadau mbalimbali katika kuhamasisha maendeleo katika eneo lake inaweza kufanya maajabu. Hata hivyo kwa masuala makubwa na vyema Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo akatumia njia za mawasialiano ya umma kwa mfano kubandika matangazo na kufanya mikutano ya jumuia. Lakini pale yanapotokea matatizo makubwa ni vyema kutumia hata vyombo vya habari pale vinapoweza kufika. Mathalani tatizo la njaa katika kata likitoka katika vyombo vya habari mamlaka zinazohusika zinaweza kuingilia kati kwa haraka zaidi kuliko mawasiliano ya chini kwa chini.


XIII. STADI ZA MAHUSIANO: Stadi za mahusiano (interpersonal skills) ni msingi muhimu sana kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweza kuleta maendeleo. Hii ni kwa sababu ukaribu wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo na watu mbalimbali ni hatua muhimu sana katika kuvutia mipango ya kimaendeleo. Pia baadhi ya miradi hutegemea mahusiano ya ukaribu kati ya Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo na wadau wa maendeleo pamoja na watendaji katika asasi hizo. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo achukulie ukaribu kama daraja la kupata fursa za kimaendeleo katika eneo lake.

XIV. KUJENGA MTANDAO NA USHIRIKA: Kuna umuhimu wa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kujenga mtandao na ushirika (network and coalition) hususani na viongozi ama wananchi wa Ubungo wengine ambao wanakubaliana katika ajenda/mipango/malengo. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo achambue masuala yanayogusa kata za jirani na kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha yanafanikiwa. Hii ni muhimu katika kujenga nguvu ya pamoja katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kimaendeleo. Pia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ajenge mtandao na ushirika na watu muhimu katika eneo lake, hii inasaidia sana katika kuongeza nguvu katika kushughulikia masuala la kimaendeleo.

XV. KUTUMIA WADAU WENGINE: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuelewa nguvu iliyoko katika kuwatumia wadau wengine. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuanza kwa kutambua wadau muhimu waliopo katika eneo lake na maeneo jirani. Lakini pia anapaswa kuwaelewa wadau wa nje ambao wanaweza kushawishiwa kufanya kazi katika eneo lake. Hii ni muhimu kwa sababu uzoefu unaonyesha kuwa kuna miradi mingi ya kimaendeleo ambayo inametekelezwa katika maeneo mbalimbali na wadau kama asasi zisizo za kiserikali, mashirika ya dini na kadhalika.

XVI. KUELEWA MIPANGO YA KISERIKALI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuielewa mipango mbalimbali ya kiserikali. Hii ni hatua muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweza kuhakikisha mipango hii inatekelezwa katika eneo lake. Baadhi ya mipango ya kiserikali ambayo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu michakato yake ni pamoja na: Mpango wa uwezeshaji kuanzia vijijini(mipango shirikishi inapangwa vijijini, WDC zinapeleka katika halmashauri-ni muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuhakikisha mipango shirikishi inapangwa ambayo ndio msingi wa bajeti);


XVII. UMUHIMU WA VIKAO: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu nguvu ya vikao katika kuleta maendeleo. Hii ni kwa sababu masuala mengi ya kimaendeleo yanahitaji maamuzi ambayo hufanyika katika vikao. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na utaratibu wa kuitisha vikao au mikutano na wanachama/wananchi kwa ajili ya kuchukua maoni, kutoa taarifa ama kujenga ukaribu. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa pia kuhakikisha kuwa anahudhuria vikao vyote muhimu anavyopaswa kuhudhuria ili kuhakikisha maslahi ya eneo lake yanazingatiwa. Kwa upande mwingine Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ahakikishe vikao vya kimaendeleo katika eneo lake vinakaa. Hivi ni vikao ambavyo vinafanya maamuzi ya msingi sana kwa ajili ya maendeleo. Ni muhimu akahudhuria vikao vya madiwani(full council) ambavyo wananchi wa kawaida wanaruhusiwa kuhudhuria.

XVIII. KUEPUKA VIKWAZO VYA KITAASISI: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na uwezo wa kuvuka vikwazo vya kitaasisi ikiwemo vya kiserikali katika kuleta maendeleo. Vikwazo viko vya namna mbalimbali mathalani urasimu, kutopewa kipaumbele, tofauti zinazotokana na misimamo nakadhalika. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuwa na mbinu za kukabiliana na vikwazo hivi. Mbinu ya msingi ni kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kufahamu vizuri haki na wajibu wake pamoja na kujua jinsi sheria na sera zinazomlinda. Pia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ajenge ukaribu na baadhi ya watendaji/wataalamu katika taasisi/serikali ili waweze kumuunga mkono. Kwa upande mwingine wale watendaji wanaoweka vikwazo lazima kuchunguza udhaifu wao na kuwabana katika udhaifu wao na kuwafanya watimize wajibu kwa hofu. Wakivuka mipaka Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anao uwezo wa kupeleka hoja wakaondolewa. Kuunganisha nguvu na wadau wengine ni njia ya ziada ya Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuruka vikwazo. Pia unaweza kutumia viongozi wa juu zaidi. Vikwazo vikifikia hatua ya juu zaidi ni vyema kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweka mambo bayana kupitia vyombo vya habari ama njia nyinginezo ili taasisi au serikali kwa ujumla wake iweze kutambua na kurekebisha hali hiyo. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutambua kuwa cha muhimu ni ujasiri. Kwenye kufuatilia haki hakuna kurudi nyuma na wakati mwingine haki haiombwi-inadaiwa.


XIX. USHIRIKI, USHIRIKISHAJI NA USHIRIKISHWAJI: Hizi ni dhana zinazorandana ambazo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuzitumia. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anao wajibu wa kushiriki katika michakato ya maendeleo. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuelewa kuwa ushiriki wake ni hatua muhimu kwa michakato hiyo kufanikiwa. Lakini pia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutulia mkazo kuwashirikisha wanachama/wananchi na wadau wengine kama msingi muhimu wa kuunganisha nguvu za pamoja. Kwa upande mwingine Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ahakikishe kwamba anashirikishwa katika mahali ambapo ni muhimu kwake lakini kwa namna moja au nyingine amesahaulika.

XX. KUJENGA IMANI KUPITIA UKWELI, UWAZI NA UWAJIBIKAJI: Kwa ujumla wanachama/wananchi na wadau wengine wa kimaendeleo katika maeneo mbalimbali wamepoteza imani na baadhi ya viongozi. Hii inawafanya wasiunge mkono kikamilifu masuala ya kimaendeleo yanayoratibiwa na viongozi hao ikiwemo katika baadhi ya maeneo kutotoa michango ya kutosha katika shughuli za kimaendeleo. Hii ni changamoto kwa viongozi na wananchi wa Ubungo. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutambua kuwa njia ya msingi ya kukabiliana na hali hii ni kujenga imani kupitia ukweli, uwazi na uwajibikaji. Kuhakikisha pesa zinatumika kwa uaminifu ni nguzo muhimu sana ya kumwezesha Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuhakikisha raslimali nyingi zaidi za kimaendeleo zinapatikana katika eneo lake.


XXI. NGUVU YA UBUNIFU NA KUCHUKUA HATUA: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu kuwa katika mazingira ya sasa ya ushindani ubunifu ni msingi wa muhimu wa kufanikiwa katika kuleta maendeleo. Mathalani pesa nyingi za miradi ya maendeleo zinatolewa kwa ushindani. Pia wakati mwingine wananchi wa eneo lake wanamtegemea Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kama kiongozi anayepaswa kutoa fikra mpya kuhusu muelekekeo wa kimaendeleo katika eneo lake. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutekeleza msingi huu. Si lazima ubunifu wote utokane na yeye, Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anaweza kuchota mawazo toka kwa watu wengine na kuyatoa katika sura yenye kuchochea mwamko na kuungwa mkono. Lakini mawazo ya ubunifu pekee hayawezi kuleta maendeleo kama hayatekelezwi. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuhamasisha na kuchochea mawazo ya ubunifu yawezwe kuwekwa katika mipango na hatimaye kutelezwa. Hivyo kuchukua hatua na kufuatilia ni nyenzo za muhimu kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuweza kuzitumia. Ukitaka kuanzisha miradi lenga katika ile inayoonekana. Na wakati wote jitahidi kuanza kwa raslimali watu. Miradi mingi inatumia mfumo wa “changa, uchangiwe”, hivyo ni vyema Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwa mbunifu wa kuanza.

XXII. KIONGOZI AMA MWANANCHI WA UBUNGO KUWA MSTARI WA MBELE NI FAIDA: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutambua kwamba uongozi na mwananchi kuwa mstari wa mbele ni faida na kwa hivyo kutekeleza wajibu kwa moyo wote na hatimaye kuleta maendeleo. Kwa upande mmoja uongozi na uanaharakati ni faida kwa jamii kwani kwa kupitia Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo maendeleo/mabadiliko yanaweza kupatikana ambayo ni manufaa kwa jamii ya sasa na jamii ya baadaye. Kwa upande mwingine uongozi na harakati ni faida kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo mwenyewe, hii ni kwa sababu inamwezesha kutambulika katika jamii, kukutana na watu/asasi mbalimbali, kupata ufahamu na kupata fursa mbalimbali za ziada.


XXIII. TUMIA MIFUMO/MIUNDO ILIYOPO: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuweka mkazo katika kuitumia mifumo/miundo iliyopo. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo aanze kwa kuchambua ni mifumo/miundo gain iliyoko katika eneo lake ambayo anaweza kuitumia. Ukweli ni kuwa katika eneo lake na nchi yetu kwa ujumla iko miundo/mifumo mingi ambayo haitumiki. Kutumia mifumo/miundo iliyopo kutamwezesha Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kupata matokeo ya kimaendeleo kwa haraka na nafuu zaidi bila kupoteza muda na raslimali za kuanzisha ama kushawishi mifumo mingine.


XXIV. NGUVU YA HOJA: Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kutambua kwamba nguvu ya hoja ni mhimili muhimu katika kufanikisha misingi yote muhimu ya kuleta maendeleo. Nguvu ya hoja inawezesha mawazo ya kimaendeleo kueleweka na kutekelezwa. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ajenge utamaduni wa kuhakikisha hoja zake zinakuwa na uzito. Ili kuwa na nguvu ya hoja ni lazima kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kuwa na taarifa za msingi mara kwa mara. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo awe mchunguzi ama mfuatiliaji. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo asiogope uchache mathalani wakati ambapo suala analolisimamia halijatokana na hoja iliyoletwa na wengi. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kufahamu kuwa cha muhimu ni nguvu ya hoja ambayo inaweza kutengeneza nguvu ya kuungwa mkono. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anapaswa kuhakikisha anazungumza kitu chenye uhakika ili kuepuka kudharauliwa au pengine hata kuchukuliwa hatua. Suala la msingi kwa Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo kusoma-sheria, kanuni, taratibu na nyaraka mbalimbali.

XXV. ENEZA TAARIFA NA ELIMU YA URAIA: Ukichambua kwa makini utagundua kuwa chanzo kikuu cha matatizo mengi miongoni mwa wananchi ni kukosa taarifa ama elimu ya uraia. Wapo wananchi wanaonyanyashwa kwa kushindwa tu kujua haki zao, wapo wanaokosa fursa za kielimu kwa kushindwa kujua wapitie hatua zipi, wapo wajane wanaonyang’anywa mirathi kwa kushindwa tu kujua jinsi ya kusimamia stahili zao, wapo waopoteza maisha kwa magonjwa kutokana na kukosa tu taarifa za msingi nakadhalika. Hivyo yapo maendeleo ambayo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anaweza kuyaleta kwa kuwezesha tu taarifa za msingi na elimu ya uraia kuenea kwa wananchi wengine. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo aweke mkazo kwa namna ya pekee sana kuhakikisha taarifa zinaenea na elimu ya uraia inatolewa. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo awe mstari wa mbele katika kufanikisha msingi huu kupitia mikutano ya jumuia, vipeperushi na njia nyinginezo. Kwa upande mwingine Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ahakikishe wadau wengine ikiwemo serikali wanatoa taarifa muhimu na kueneza elimu ya uraia kuhusu fursa na michakato mbalimbali ya kimaendeleo.

Rejea:

• John Mnyika, Misingi 29 ya Vijana Kuleta Maendeleo Katika Maeneo yao-2007
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
• Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, 1948(UDHR).
• Ushiriki wa Wananchi katika Serikali za Mitaa, 2005(Policy Forum)
• Sheria ya Serikali za Mitaa, 1982

Thursday, January 17, 2008

Barua ya wakazi wa Kibamba

WAATHIRIKA WA UHAMISHWAJI KIMABAVU LUGURUNI NA KIBAMBA HOSPITALI (WUKILUKI).
wukiluki.kibamba@yahoo.com

03 Januari, 2008
Waziri
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi

Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi

Mkuu wa Mkoa
Mkoa wa Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya
Wilaya ya Kinondoni

Mkurugenzi
Manispaa ya Kinondoni

Yah: KUOMBA MENEJA WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDO MBINU LUGURUNI NA KIBAMBA HOSPITALI AWAJIBISHWE KUTOKANA NA KUKITHIRI KWA VITENDO VYA RUSHWA, MALIPO YA FIDIA HEWA, BAADHI YA WATU KUZIDISHIWA KIWANGO CHA MALIPO YA FIDIA ISIVYO HALALI NA MENEJA WA MRADI KUWATISHA WATU WATOA HABARI JUU YA VITENDO HIVYO VICHAFU.

Rejea katika mazungumzo kati ya mwakilishi wa waathrika wa mardi huu na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, yaliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Desemba 2007, yakihusu madai ya kuwepo malipo ya fidia hewa na watu kuzidishiwa malipo ya fidia isivyostahili.

Kwa mujibu wa majibu ya Kaimu Katibu Mkuu kwa mwakilishi wa waathrika baada ya kikao cha uchunguzi kuitishwa, Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa wizara itasimamisha malipo kwa majina yaliyowasilishwa wizarani yakidaiwa kuwa ni malipo hewa. Pia Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa imeamuliwa kuwa uhakiki wa malipo ya fidia katika mradi huu utafanyika mara moja.

Sisi waathrika tunapenda kuipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi kwa kuchukua hatua za haraka ili kuokoa fedha za serikali zisipotee. Kasi hiyo ya ajabu imeijengea heshima kubwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi pamoja na viongozi wake.

Kutokana na uamuzi huo wa wizara, matendo yafuatayo yalifuatia yenye lengo la kukwamisha azma ya wizara kuokoa fedha za serikali, kuwatambua na kuwanasa wote waliolipwa fidia isvyo halali. Vitendo hivyo ni pamoja na:-

1) Waliohusika kulipwa malipo hewa kuonekana kushughulika kutafuta ardhi na majengo ya kuonyesha wakati wa zoezi la uhakiki. Hii ikashiria ya kuwa tayari wafanya uhakiki (wale wale waliohusika) wamearifiwa kufanya hivyo ili kuficha uovu.

2) Uongozi na watendaji wa mradi kuonekana mara kwa mara eneo la mradi wakati wa sikukuu za krismai na mwaka mpya wakizunguka zunguka na wanaodaiwa kulipwa malipo hewa na wanaodaiwa kuzidishiwa malipo isivyo halali.

3) Meneja wa mradi kuwapigia simu na kuwatishia Ndg Selestine Michael na Mama Edgar walionekana wakitoa malalmiko yao katika kituo cha ITV kuwa watabomolewa pasipo kulipwa fidia yoyote. Vitisho hivi vilikuwa na ari wa wananchi kutoa taarifa zaidi za vitendi viovu.

Kwa mujibu wa vitendo vilivyofuatia uamuzi huo wa serikali, sisi waathrika tuna kila sababu ya kuamini kuwa vitendo vya rushwa, malipo ya fidia hewa na baadhi watu kuzidishiwa malipo isivyo halali vilifanyika kwa ufahamu na baraka za uongozi wa mradi huu (Meneja), na ndio maana baada ya wizara kuagiza uhakiki ufanyike vitendo vya kupoteza ushahidi na kujaribu kuwanyamazisha watoa habari vinafanyika.

Tunalazimika kusema hivyo kwa kuwa meneja huyu aliwaruhusu maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini mali (Valuers) walio chini yake kuwatumia madalali wa viwanja na nyumba katika kutambua maeneo na kuthibitisha wamiliki halali badala ya kutumia Ofisi ya serikali za Mitaa. Kutumika kwa madalali badala ya ofisi ya serikali ya kulifanyika kwa nia ya kufanikisha malipo hewa kwa kuwa dalali huyu anatambua mashamba na viwanja ambavyo wamiliki aidha wamefariki, kuwa nje ya nchi au kukaa muda mrefu pasipo kuhudumiwa.

Maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali waliokuwa chini ya meneja huyu walimtumia sana dalali wa viwanja aitwaye Ndugu Norbert Mtewele (Mbenna) kinyume na sheria za ardhi. Dalali huyu ni mjumbe wa shina eneo la Kibamba hospitali lakini aliweza kutumika na watekelezaji wa mradi huu hadi maeneo ya Luguruni, Msakuzi na Kibamba CCM na katika Mitaa ya Kwembe na Kiruvia kutambua maeneo na kuthibitisha uhalali wa wamiliki badala ta ofisi za serikali ya Mitaa husika.

Kama ujira wa dalali huyu, maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali wa mradi huu walimpatia dalali Morbert Mtewele malipo ya fidia katika jengo lililopo katika barabara ya zamani ya Morogoro, wafanyabiashara wengine zaidi ya 30 katika eneo hilo hilo walinyimwa fidia hiyo kwa kuwa barabarani. Aidha inadaiwa kuwa dalali huyu alipatiwa fidia inayozidi thamani ya jengo husika kwa zaidi ya mara 10.Vile vile inadaiwa kuwa watekelezaji wa mradi huu walitumia majina ya wadogo wawili wa dalali huyu wajulikanao (majina tunayahifadhi) kujipatia fidia isiyostahili kwa kutumia viwanja na majengo wasiyo kuwa wamiliki halali. Inakadiriwa kuwa kisai cha zaidi ya shilinngi million 40 za serikali zinazotosha kujenga madarasa 5 (tano) zimepotea kwa watu hawa watatu tu.

Sisi waathrika wa mradi huu tanaamini kwa dhati ya kuwa azma ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ya kuokoa fedha za serikali na kuwatambua watu waliolipwa isivyo halali haitafanikiwa kutokana na kukiukwa kwa “Natural Justice” katika zoezi zima la uhakiki wa malipo ya fidia ndani ya mardi huu. Haiwezekani mtendaji aruhusu/afanikishe/afanye malipo hewa halafu ajihakiki mwenyewe. Pia azma hiyo haitatekelezeka kwa kufanya uhakiki wa zima moto kwa watu waliotyajwa tuu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa kamati yetu orodha ya watu waliohusika kulipwa malipo hewa na watu kulipwa zaidi kuliko wanavyostahili ni ndefu na itahusisha kiwango kikubwa sana cha fedha za serikali kupotea. Upo ushahidi unaoonyesha ya kuwa wapo watu ambao hawakuwa wakazi wa Kibamba kabisa ambao wamelipwa fidia na kutokomea na fedha za serikali isivyo halali. Na hii itathibitika tu pale uhakiki kamili utakapo fanyika na kuwabainisha wazi wazi kwa kuwa hadi sasa hakuna muathirika hata mmoja ambaye ameweza kuhama. Orodha iliyowasilishwa wizarani, ni ya watu wachache tu walioanza kutajwa tajwa na wananchi kuwa walihusika na vitendo hivyo.

Hivyo basi ili azma ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ya kuokoa fedha za seriakli itimie, ipo haja ya wananchi kujengewa mazingira muafaka ya kuendelea kuwataja wahusika wote waliohusika na kulipwa fidia isivyostahili, wakiwemo maafisa ardhi waliohusika kuomba rushwa ili waweze kuwasaidia wananchi watakaokumbwa na mradi huu waendelee kubaki walipo bila ya kuhamishwa. Pia maafisa tathmini mali (Valuers) waliokuwa wakiomba rushwa ili waweze kuwaongezea watu malipo ya fidia kuliko wanavyostahili na wale waliohusika kufanikisha malipo ya fidia hewa.

Ili kuweza kujenga mazingira muafaka ya wananchi na waathrika kuwa na ujasiri wa kuwataja wote waliohusika na vitendo hivyo, ipo haja kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za makusudi zitakazo onyesha wazi wazi kuwa uongozi wa taasisi unataka kupambana na vitendo vya namna hii katika mradi huu na miradi mingine yote ya namna hii itakayofuata. Kwa kuwa hata mtukufu Rais jakaya M kkwete alishaonyesha wazi wazi kukerwa na kukuthiri kwa rushwa miongoni mwa watendaji wa masuala ya rdhi hapa nchini. Sisi waathrika tunapendekeza kuwa uhakiki wa malipo ya fidia ufanywe na watu tofauti na wale ambao wakihusika katika kujenga mazingira ya kufanikisha malipo hewa ya fidia n.k. Vile vile tunaomba wale wote waliohusika na kutowajibika ipasavyo hadi vitendo hivi vikatokea wawajibike mara moja ma wasihusike katika uhakiki wa malipo ya fidia ili kuweza kujenga uwazi na kuleta imani katika zoezi zima la uhakiki wa malipo ya fidia.

Sisi wananchi na waathrika wa mradi huu tunashauri kuwa endapo zoezi la uhakiki litawahusisha watendaji wale wale waliohusika kufanikisha vitendo viovu vilivyotajwa hapo juu ni wazi kuwa wananchi hawatakuwa tayari kuwataja wote waliohusika na matendo haya. Hivyo fedha za serikali hazitaweza kuokolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni hazitaweza kuwabaini watendaji wanojihusiha na vitendo vya rushwa na kukiuka taratibu za utendaji kazi katika masuala ya uboreshaji makazi yasiyopimwa.

Kutobainika kwa watendaji hawa wabovu kutapelekea vitendo vya aina hii kuendelea kushamiri katika masuala yanayohusu uboreshaji makazi yasiyopimwa na fedha nyingi sana za serikali kuendelea kupotea. Pia kutobainika kwa watendaji hawa wabovu ili waweze kuondolewa kutapelekea kuendelea kufedheheshwa kwa serikali mbele ya wananchi wake, ambao wanatazamia kupata huduma safi kutoka kwa watumishi wa serikali badala ya kuombwa rushwa, kupunjwa malipo ya fidia kutokana na kuwepo vitendo vya malipo hewa na baadhi ya watu kuzidishiwa malipo isivyo halali.


Ahsante
Majina sahihi zetu hapo chini


Waathrika wa Uhamishwaji Kimabavu Luguruni na Kibamba Hiospitali
(WUKILUKI)






Nakala

1) Mhe Jakaya M Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


2) Mhe Edward Lowassa
Waziri Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu


3) Mhe Mizengo Pinda
TAMISEMI


4) Taasisi ya Kuzuia Rushwa
Wilaya ya Kinondoni

Tuesday, April 03, 2007

UDI yatambulishwa rasmi!

UDI YATAMBULISHWA RASMI
Programu ya UbungoTaarifa yaanza kutekelezwa

Hii ni taarifa rasmi kwa umma kuitambulisha Ubungo Development Initiative (UDI)- Asasi ya Maendeleo Ubungo. UDI ni asasi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa rasmi mwishoni mwa mwaka 2006. Dira ya UDI ni kuchangia katika kuleta maendeleo ya jimbo la Ubungo na maeneo jirani. UDI inatimiza wajibu huu kwa kuhamasisha uwajibikaji wa wananchi, viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo. UDI inaweka mkazo zaidi katika uwezeshaji, ujasiriamali na elimu ya uraia.

Kwa kuanzia kwa mwaka huu wa 2007, UDI inatekeleza programu ya UbungoTaarifa. Hii ni programu inayohusisha kukusanya na kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo. “ Tunatambua kwamba jimbo la Ubungo liko katika mkoa wa Dar es salaam ambao unafursa nyingi sana ambazo hajitumika bado. Yapo mashirika ambayo yanatoa msaada wa kisheria. Zipo taasisi zinazotoa mikopo. Na zipo taasisi mbalimbali ambazo zinafanya shughuli mahususi za kimaendeleo. Lakini wananchi waliowengi katika jimbo la Ubungo hawafahamu huduma zinazotolewa na taasisi hizi. Programu ya UbungoTaarifa inalenga kuwafahamisha uwepo wa huduma hizo. UDI itakuwa kiungo kati ya mashirika hayo na wananchi katika mwaka huu 2007”. Kuanzia mwaka 2008 na kuendelea UDI itazindua programu zingine za kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo ambayo kuna uhaba wa huduma.

Pia, UDI inapenda kuujulisha umma kwamba Taarifa yake ya Fedha kwa mwaka 2006 imeshafanyiwa ukaguzi wa mahesabu na wanachama na wananchi kwa ujumla wanaweza kuipitia. Aidha UDI inatumia fursa hii kutoa mwito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuweka wazi mapato na matumizi yao kama sehemu ya kuchochea uwajibikaji.

Wakati, huo huo- UDI inatoa mwito kwa watanzania kuwasaidia mitaji watanzania wenzao wasio na uwezo. “ kama kila mtanzania mwenye uwezo akimsaidia mtanzania mmoja tu mabadiliko ya hali ya juu yatatokea katika maisha ya watu wengi”. Hii imedhihirika kutokana na mfano wa Mama Halima Rashid ambaye ameomba kuambatana na UDI kutoa ushuhuda wake baada ya kusaidiwa na Kijana wa Kitanzania James Kitia aliyeko Ohio Marekani. Kijana huyu alisoma kwenye vyombo vya habari vya nyumbani kwa njia ya mtandao habari za Mama Halima ambaye alikimbiwa na mumewe baada ya kuwa na mtoto mwenye ulemavu na hivyo akakosa kabisa matunzo yake na ya mtoto. Baada ya kusoma habari yake James aliamua kumpatia mtaji kidogo wa shilingi laki mbili kupitia kwa mmoja wa waasisi wa Asasi ya Maendeleo Ubungo(UDI) Bwana John Mnyika. Bwana Mnyika alimkabidhi mchango tarehe 8 mwezi wa Machi, 2007 ambayo kwa bahati ilikuwa ni siku ya wanawake duniani. Leo ikiwa imepita takribani mwezi mmoja toka apatiwe mtaji huo ambao ameuelekeza katika biashara ya kuuza mayai kwa jumla na magazeti, Mama Halima yuko tayari kutoa ushuhuda wa mabadiliko ambayo mchango huo kidogo umeleta katika maisha yake.


Pia, UDI kama asasi inayosimamia uwajibikaji na maendeleo Ubungo na Tanzania kwa ujumla imefuatwa na kijana mkazi wa Jimbo la Ubungo katika kata ya Sinza Bwana Alistides Huntergration Buberwa ambaye amefungua kesi katika mahakama kuu kupinga Umri wa Kugombea Urais kuwa miaka 40 na fomu za Urais na Ubunge kutolewa gharama kubwa kuliko uwezo watanzania walio wengi hususani vijana. Katika kesi hiyo Alistides amepewa msaada wa Kisheria na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC). UDI kama asasi inayotoa sauti kwa wananchi katika masuala ya kimaendeleo imeamua kumpatia fursa hii aitambulishe kesi hiyo kwa umma.


Mwisho, UDI inaomba kuchukua fursa hii kuomba ushirikiano wa wananchi wa Ubungo, Serikali, Sekta binafsi na wadau mbalimbali wa kimaendeleo katika kutekeleza programu ya UbungoTaarifa na shughuli nyingine za kuhamasisha uwajibikaji na maendeleo katika jimbo Ubungo na maeneo jirani.


Wenu katika ujenzi wa Taifa



Harold Makundi
Katibu Mtendaji
3/4/2007

Sunday, October 01, 2006

UDI intro!

UDI INTRODUCTION

Ubungo Development Initiative (UDI) is a civil society organization established and registered in Tanzania in 2006. There was no civil society organization that is focusing to promoting development in the Ubungo community and its vicinities. The founders of the organization realized during 2005 that development of the constituency can be expedited with good leadership and responsible citizenry that necessitate civic society advocacy and service. The organization is operating within the philosophy of U-26 that translates to Ubungo, leadership, representation, involvement, transparency, citizenry, responsibility, research, planning, implementation, monitoring, advocacy, lobbying, empowerment, knowledge, participation, accessibility, truth, security, cleanliness, transport, entrepreneurship, employment, economy, welfare and freedom. The organization is complimenting the efforts of the residents, government and other stakeholders for the development of Ubungo community and its vicinities through enhancing responsibility, empowerment, entrepreneurship and freedom.

Generally the objectives of UDI are:

(a) To enhance the socio-economic status of people through appropriate empowerment programmes that facilitates the realization of their potentials and opportunities.

(b) To stimulate broad public engagement, information sharing and dialogue on empowerment and related matters in pursuit of creating a movement for social and economic change.

(c) To promote responsible citizenry, strategic preparation of the people to take a role in leadership and ensure good governance.

(d) To enable people acquire knowledge and conceptual capacity through dialogue, information generation and sharing.

(e) To implement pilot service and development programs and activities particularly through networking and collaboration.

(f) To facilitate the development of private and informal sectors;